TWCC yaandaa Tuzo za Viwanda

TWCC yaandaa Tuzo za Viwanda

CHAMA cha Wanawake wenye Viwanda na Biashara nchini  (TWCC) kimeandaa tuzo za viwanda ili kuchochea maendeleo katika jamii.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Salaam, Mkurugenzi wa TWCC Mwajuma Hamza, amesema kuwa wanawake wamekuwa nguzo muhimu katika maendeleo hasa viwanda na kueleza kuwa kutakuwa na maonesho kuanzia Machi 9-12, mwaka huu ukumbi wa Mlimani City na mwishoni mwa maonesho hayo ndipo kutakuwa na tuzo.

“Wanawake wanaweza kufanya mapinduzi makubwa kwenye sekta ya viwanda endapo wataaminiwa na kuaminika na kupewa nafasi,”amesema Mkurugenzi huyo.

Advertisement

Amesema serikali imekuwa ikiwezesha mazingira ya biashara kwa wanawake katika uanzishwaji wa biashara na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha wa mazingira yao ya uwekezaji nchini.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Trade Mark nchini, Monica Hangi amesema kuwa shirika hilo limetenga zaidi ya Sh billioni 4 ili kufanikisha miradi mbalimbali ya kuwajengea uwezo wanawake.

“Tuzo hizi zina lengo la kuhakikisha biashara za wanawake nchini zinakuwa na kuleta tija kwa taifa,”amesema.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *