Twendeni tukaujaze!

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kushuhudia michezo miwili ya michuano mipya ya African Football League (AFL), itakayochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Dk Ndumbaro amesema ni heshima kwa nchi kuaminiwa na kuteuliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa michuano ya AFL kuzinduliwa kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Tanzania, ambapo Simba SC ya Dar es Salaam itavaana na Al Ahly ya Misri.

Advertisement

Aidha, kiongozi huyo amesema Tanzania imepewa nafasi ya kuwa mwenyeji wa mchezo wa pili AFL kutokana na wakaguzi wa CAF kuvutiwa na utendaji unaofanyika nchini sambamba na huduma bora zinazotolewa ikijumuisha maeneo bora ya viwanja vya michezo, huduma bora za hoteli, usafirishaji salama wa abiria na mizigo.

“Mechi kati ya TP Mazembe DRC dhidi ya Esperance ya Tunisia iliyopaswa kuchezwa pale Lubumbaji, imehamishiwa Dar es Salaam, tumepewa sisi Tanzania na utapigwa Uwanja Benjamin Mkapa, na utachezwa Oktoba 22, 2023,” amesema Dk Ndumbaro.

Amesema ujio wa AFL nchini ni fursa kwa sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya utalii, sekta ya michezo, sekta ya biashara na uimarishaji wa masuala ya kijamii na kidiplomasia.

2 comments

Comments are closed.