Twiga Stars ndio basi tena!

MPUMALANGA, Afrika Kusini: BAO la mshambuliaji wa timu ya taifa ya Wanawake ya Afrika Kusini, Thembi Gatlana katika dakika 58′ limezima ndoto ya Twiga Stars kushiriki michuano ya Olimpiki mwaka huu nchini Ufaransa.

Twiga Stars imekubali kipigo cha bao moja kwa sifuri usiku wa kuamkia leo katika Uwanja wa Mbombela, Nelspruit Mpumalanga nchini Afrika Kusini na kufanya matokeo ya jumla kuwa bao 4-0 baada ya mchezo wa awali katika Uwanja wa Chamazi complex jijini Dar es Salaam, juma lililopita kukubali kipigo chamabao 3-0.

Kwa matokeo haya, Banyana Banyana watavaana na Nigeria ‘Super Falcons’e mwezi Aprili mwaka huu katika mzunguko wa kumpata muwakilishi pekee wa Afrika upande wa timu za mpira wa miguu kwa wanawake katika mashindano ya Olimpiki yanayotarajiwa kuvurumishwa kuanzia Julai 24 hadi Agosti 10 jijini Paris.

Habari Zifananazo

Back to top button