Twiga Stars yatakata na kusonga mbele

DAR ES SALAAM: TIMU ya Taifa ya wanawake Twiga Stars imesonga mbele katika kampeni ya kuisaka tiketi ya kucheza michuano ya mataifa ya Afrika kwa Wanawake ya mwaka 2024 (WAFCON 2024) itakayofanyika nchini Morocco.

Twiga Stars ikiwa nyumbani katika dimba la Azam Complex imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ivory coast ushindi uliofanya matokeo ya jumla kuwa sare ya mabao mawili baada ya Ivory Coast kushinda mchezo wa juma lililopita wakiwa nyumbani.

Mabao ya Stars katika mchezo huo yamefungwa na Donisia Minja na Opah Clement mapema kipindi cha pili.

Baada ya sare hiyo mchezo huo umeamuliwa kwa mikwaju ya Penati ambapo Twiga Stars wameibuka na mikwaju 4-2, na sasa wanamsubiri mshindi wa jumla kati ya Togo na Djibouti ili kumfahamu mpinzani wake.

Hata hivyo uwezekano mkubwa ni kuwa Twiga Stars inaweza kucheza na Togo kutokana na faida ya matokeo aliyopata Togo dhidi ya Djibouti katika mchezo wa mkondo wa kwanza.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x