Twiga yavuliwa ubingwa Cosafa

TIMU ya soka ya Taifa ya Wanawake, ‘Twiga Stars’ imevuliwa ubingwa mashindano ya Cosafa baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka Zambia kwenye Uwanja wa Isaac Wolfson, Port Elizabeth jana.

Katika mchezo huo wa nusu fainali, Zambia walianza kupata bao dakika ya 12 likifungwa na Barbara Banda. Wakionesha wanataka kulipa kisasi cha kufungwa na Twiga Stars katika nusu fainali za mashindano hayo mwaka jana, Zambia waliendelea kulishambulia lango la Tanzania lakini kipa Najiat Abbas alijitahidi kuokoa hatari zote.

Twiga Stars hawakuonesha unyonge licha ya Zambia kuwa na wachezaji wake wote wanaokwenda kucheza Fainali za Kombe la Dunia waliliandama lango lao na kumfanya beki wao Agness Musese kujifunga akiwa kwenye harakati za kuokoa na kufanya timu zote kwenda mapumziko zikiwa sare ya 1-1.

Kipindi cha pili Zambia walianza kwa kasi na kuongeza bao la pili dakika ya 46 likifungwa na Shisha Misozi lakini hata hivyo Twiga Stars waliendelea kucheza mchezo mzuri na wa kiufundi.

Twiga Stars sasa itacheza mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu kesho dhidi ya Namibia huku Zambia ikicheza fainali na Afrika Kusini​​​​​​​.

Habari Zifananazo

Back to top button