Twitter kufanya mabadiliko mengine tena

TWITTER imesema inatarajia kuongeza kipengele kipya kwenye jukwaa hilo kitakacho onesha idadi ya watu waliopita na kuona chapisho (tweet) mtumiaji wa jukwaa hilo la kijamii, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu Elon Musk alitangaza Alhamisi. 

Kasi ya bosi huyo mpya kuweka vipengele vipya katika jukwaa hilo umekosolewa tangu alipoinunua Twitter kwa dola bilioni 44 mwezi Oktoba.

Kipengele hicho, ambacho tayari kipo kwa ajili ya video, kitaonyesha “ni kiasi gani Twitter iko hai kuliko inavyoweza kuonekana,” Musk aliandika, akifafanua kwamba “zaidi ya asilimia 90 ya watumiaji wa Twitter wanasoma, lakini hawa- tweet, kujibu au kuonesha hisia (like) kama matendo ambayo yako wazi.”

Advertisement

Muda mfupi baada ya kununua Twitter, Musk alisema kuwa marekebisho yake ya jukwaa yatahusisha “mambo mengi.” Kufikia sasa, ameanzisha, kughairi, kurekebisha, na kurejesha mfumo wa uthibitishaji kwa kulipia, kabla ya kutangaza na kisha kufuta mipango ya kusimamisha akaunti zinazo linganisha tovuti za kijamii zinazoshindana.

Musk aliyejitambulisha kama “mtetezi huru wa kujieleza,” pia alirejesha akaunti iliyopigwa marufuku ya Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, na akatoa data nyingi zinazoonyesha kuwa chini ya usimamizi wa zamani, Twitter ilishirikiana na FBI kuondoa na kuhakiki habari ambazo shirika hilo lilitaka kufichwa.

Licha ya kuingiza mapato mengi Twitter na msukosuko wa habari kuhusu ununuzi wake wa Twitter, Musk alidai mwishoni mwa mwezi uliopita kwamba usajili wa watumiaji wapya umefikia “kiwango cha juu kabisa.”

Siku ya Jumanne, Musk alitangaza kwamba atajiuzulu kama Mkurugenzi Mtendaji wa Twitter mara tu atakapo pata ‘mtu makini’ wa kuchukua nafasi hiyo.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *