Ubalozi wa Uswidi nchini wazindua lori la gesi asilia

DAR ES SALAAM: KATIKA kuadhimisha miaka 60 ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Uswidi, Ubalozi wa Uswidi nchini umezindua kampeni ya kuhamasisha matumizi ya nishati rafiki kwa mazingira katika usafirishaji ili kulinda mfumo wa ikolojia nchini na kukabiliana mabadiliko ya tabianchi.

Hayo yameelezwa leo Oktoba 02, 2023 na Balozi wa Uswidi nchini, Charlotta-Ozaki Macias jijini Dar es Salaam, wakati akizindua ziara ya kusafiri kwa usalama ‘The Clean Transport Tour’ kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa kutumia lori linalotumia nishati ya gesi asilia.

“Tanzania na Uswidi kwa muda mrefu imekuwa na mahusiano mazuri katika kila nyanja ya kimaisha kwa takribani miaka 60 sasa ikiwemo katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Kuna matokeo mengi chanya ya kujifaharisha nayo, ambapo pia tumejifundisha namna bora ya kufanikiwa siku za usoni,” amesema Macias.

Aidha, kupitia ziara hiyo inayoratibiwa na Ubalozi wa Uswidi kwa kushirikiana na Kiwanda cha Kiswidi cha utengenezaji wa magari ya Scania,

Mkurugenzi Mtendaji wa Scania nchini, Ali Dar amesema lori la gesi la scania limefuata utaratibu wa matumizi sahihi ya nishati rafiki kwa mazingira, injini ya Euro 6, inayofanya kazi kwenye gesi asilia iliyobanwa kwa hiari au biogas.

“Lori hili la Scania lilizinduliwa rasmi nchini Tanzania mwaka 2021, ni lori la kisasa linaloenda sambamba na mabadiliko ya kiteknolojia ambalo litatumia gesi asilia (CNG) lakini pia gharama zake ni nafuu kulinganisha na lori linalotumia mafuta,” amesema Dar.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button