‘Ubaya wa mwanaume unatengezwa na shetani’

MTWARA; WANAWAKE wametakiwa kufahamu kuwa hakuna mwanaume mbaya, bali ubaya unaonekana kwa baadhi ya wanaume unatengenezwa na shetani.

Mtumishi na Mwalimu wa neno la Mungu, Joyce Kangonji amesema hayo wakati akifundisha neno la Mungu katika semina ya wanawake ambayo imeandaliwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Ushirika Kanisa Kuu Mtwara.

Mtumishi na Mwalimu wa neno la Mungu Joyce Kangonji

“Hakuna mwanaume mbaya, ubaya kwa mwanaume unatengenezwa na shetani,” amesema.

Mwalimu Joyce amesema wanawake wanapaswa kujua hilo na kutambua na kuishi katika misingi ya kimungu ambayo inawataka wanawake kuwa walinzi na wasaidizi kwa mwanaume.

Amesema wanawake wakiishi kwa misingi ya kimungu wakizingatia kuwa wao ni walinzi na wasaidizi kwa wanaume wao shetani, hatapata nafasi ya kuingiza ubaya kwa mwanaume.

Habari Zifananazo

Back to top button