‘Ubora dawa za viuadudu mbovu, mbaya sana’

DODOMA; NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Azzan ‘Zungu’, amesema dawa nyingi za cha viuadudu kutoka nje ya Tanzania zina ubora mdogo, mbovu na ni mbaya sana.

Ametoa kauli hiyo bungeni leo, baada ya Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel kumaliza kujibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Rose Tweve aliyehoji kwa nini serikali isiwekeze fedha kiwanda cha viuadudu Kibaha ili kutokomeza malaria nchini.

“Hizi dawa za viuadudu nyingi zinaagizwa kutoka nje, ubora wa dawa hizo ni mdogo, mbovu na mbaya sana.Kiwanda hiki kipo nchini mwetu,” amesema na kushauri sasa wanunue vitu katika viwanda vya ndani na kuongeza kuwa:

“Nunueni vitu ndani ya Tanzania, itaokoa pesa za kigeni, itaokoa kuingiza madawa ambao hayana ubora, Waziri wa Viwanda na Biashara uko hapa, TBS wahakikishe, haya madawa mengi yanayotoka nje hayana ubora wowote,” amesema Naibu Spika.

Akijibu swali la msingi Naibu Waziri Mollel, katika kipindi cha mwaka 2017 hadi 2023, Serikali imenunua viuadudu vyenye thamani ya shilingi bilioni 5.9 na kutumika katika ngazi ya Halmashauri.

“li kuhakikisha uhakika wa upatikanaji wa viuadudu kutoka kiwanda cha Kibaha, kwa kipindi cha mwaka 2024-2026, Wizara ya Afya imeomba kupatiwa jumla ya Shilingi bilioni 129.1 kwa ajili ya utekelezaji wa afua ya unyunyiziaji wa viuadudu ili kuangamiza viluilui wa mbu kwenye mazalia ili kufikia lengo la kutokomeza malaria ifikapo 2030.

“Mheshimiwa Spika, Wizara ya Afya inashirikiana na Shirika la Taifa la Maendeleo ya Viwanda kuhakikisha kiwanda kinapata ithibati kutoka Shirika la Afya Duniani, ili kuongeza wigo wa upatikanaji wa fedha za kutekeleza afua hii kutoka kwa wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria,” amesema Naibu Waziri huyo.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Tibirizi Chakechake Pemba
Tibirizi Chakechake Pemba
23 days ago

Hela za kujenga ofisi za serikali zimepungua kwa asilimia 100, manager lini tutasini vifone = ajira zitaongezeka kwa asilimia 300

Capture2.JPG
Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x