Ubungo yakusanya Sh Milioni 367 uandaaji hatimiliki

DAR ES SALAAM: WILAYA ya Ubungo jijini Dar es Salaam imekusanya Sh milioni 367 ikiwa ni kodi itokanayo na ada na tozo mbalimbali za uandaaji wa hati miliki.

 

Mratibu wa Urasimishaji Mkoa wa Dar es Salaam, Laurent Mswani amesema hayo alipotoa taarifa ya utekelezaji ukwamuaji wa urasimishaji wa awamu wa kwanza katika Halmashauri ya Ubungo, ulioanza Novemba 13 mwaka huu na kutarajiwa kuhitimishwa leo mchana.

Advertisement

 

“Kupitia huduma hii jumla ya maombi ya hati 1898 yalipokelewa na kuchakatwa na hati 1,692 zimetolewa  sawa na asilimia 89.2 ya maombi yaliyopokelewa.

 

“Jumla ya changamoto 798 zinazohusu urasimishaji zilipokelewa na kusikilizwa,” amesema Mswani.

 

Amesema katika huduma hiyo wananchi 2692 wamepatiwa huduma mbalimbali za ardhi ikiwa ni pamoja na kuandaliwa hati miliki, kupewa elimu ya masuala mbalibali  ya ardhi pamoja na kusikilizwa na kutatua chsngamoto  mbalimbali  za urasimishaji.

 

Amesema kati ya hati hizo zilozoandaliwa na kusajiliwa 1,692. Hati 552 zimetolewa kwa wanaume, hati 328 zimetolewa kwa wanawake, hati 93 umiliki wa pamoja, hati 17 kampuni na nane ni taasisi.

 

Amesema changamoto 798 zinazohusu masuala mbalimbali ya ardhi zimeweza kusikilizwa, zikiwemo changamoto zilizojitokeza katika huduma hiyo kuwa ni kuwepo kwa idadi kubwa ya wananchi ambao upiaji wa maeneo yao haujakamilika, pia kuwepo kwa hali ya hewa ya mvua ambayo ilisimamisha utoaji wa huduma kwa vipindi tofauti. Ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa vitendea kazi vya kisasa pamoja na changamoto za mtandao.

 

“Kupitia dawati la kusikiliza changamoto hizo jumla ya changamoto 528 zimepatiwa majibu, 105 bado zinaendelea kufanyiwa kazi na 165 ni migogoro ambayo inaendelea kusikilizwa katika vyombo vya sheria ” amesema kiongozi huyo.

 

Ameeleza mikakati pendekezi ili kufanikisha mpango wa kuboresha hudumaza ardhi na kujwamua kazi za urasimishaji kuwa ni kuunda timu za wataalam wa ardhi. Ikiwa na kuendelea kutekeleza mpango wa ardhi kliniki ili kuongeza kasi ya hudumaza ardhi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *