Ubunifu kuongeza soko wafanyabiashara Kagera

MKUU wa Wilaya ya Bukoba, Erasto Sima ametoa wito kwa wanawake wafanyabiashara kufanya ubunifu katika biashara zao ili kukabiliana na changamoto ya masoko yaliyopo ndani na nje ya nchi.

Aliyasema hayo wakati akifunga mafunzo kwa wanawake 36 mkoani Kagera ambao wamehitimu mafunzo ya Ujasilimia AWE (Academy for Women Enterpreneurs) yaliyofadhiliwa na ubalozi wa marekani kwa lengo la kuwawezesha wanawake wa mikoa ya pembezoni kuzifikia fursa za kibiashara zilizowazunguka.

Alisema kuwa kwa sasa wafanyabiashara wengi wangeongezeka hivyo swala la ubunifu katika biashara ni muhimu hasa uboreshaji wa bidhaa,kuongeza thamani,ubora wa kifungashio na mwonekano wake.

“Kila mmoja anandoto ya kufanya Biashara na serikali imeongeza wigo wa kufanya biashara katika nchi mbalimbali lakini Kama Mfanyabiashara ambaye umepata Mafunzo unayatumia vipi mafunzo hayo kuongeza ubunifu katika Biashara yako na kujipatia wateja wapya ?? lazima tubadili mifumo ya biashara zetu “alisema Sima.

Askofu wa KKKT Dayosisi ya kaskazini Magharibi Abednego Keshomshahara ambaye alipata Nafasi ya kuudhuria shereh za kuhitimu Mafunzo hayo alisema kwa Sasa kunamabadiliko makubwa kwa kundi la wanawake ambao wamejiongezea maarifa katika Biashara na migogoro katika Familia inapungua kwa sababu wanajipatia kipato.

Alisema kuwa anaamini Baada ya Mafunzo haya ya ujasiliamali kwa wanawake 36 mamia ya wanawake wanaoishi maeneo ya pambezoni mkoani Kagera watapata Elimu ya ujasiliamali kwa wanawake wenzao na wao watazifikia Fursa za masoko katika nchi za Afrika Mashariki zilizouzunguka mkoa wa Kagera.

Mratibu wa Kitengo cha ujumuishaji wa jamii kutoka ubalozi wa Marekani nchini Tanzania Rehema Kalinga alisema kuwa lengo la Mafunzo hayo ni kuhakikisha wajasiliamali wadogo wanakua katika Biashara zao na wanakuwa wafanyabiashara wakubwa hivyo kuzifikia ndoto hizo ni lazima waongezeae maarifa ya elimu hasa kwa Lugha ya kingereza na kiswahili zinazotumika katika biashara kwa nchi za Afrika Mashariki.

Alisema kwa mwaka 2023 mafunzo haya ya ujasiliamali yamefanyika mikoa ya Kigoma na Kagera na wanawake ambao walipata nafasi ya kushiriki mafunzo wanajifunza namna ya kuanzisha biashara, namna ya kuagiza bidhaa na kuuza nje ya nchi,namuna ya kuyafikia masoko ya kimataifa ,kushiriki maonyesho ya kimataifa ya kibiashara pamoja na kuwa chachu katika jamii kwa kuwaelekeza wanawake wengine nna ya kufanya biashara.

Mafunzo ya ujasiliamali kwa wanawake mkoani Kagera ambayo yaliratibiwa na shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na kuleta ujumuishaji wa matumizi ya digtali katika mikoa ya pembezoni Tanzania Omuk Hub yamefanyika kwa wiki 12 Kati ya hizo wiki mbili zilitumika kufundisha somo la Kingereza ili kuwasaidia wajasiliamali kupambana na lugha za kibiasha katika masoko.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button