‘Ubunifu ni chachu ya maendeleo nyanja zote’

DAR ES SALAAM; WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), unaadhimisha siku ya miliki bunifu, ambayo pia inaonesha namna nchi inavyoweza kutambua mchango wa wabunifu kuleta maendeleo.

Mkurugenzi wa miliki bunifu kutoka Brela, Loy Mhando amesema hayo leo wakati akizungumzia maadhimisho hayo yatakayofanyika kesho Dares Salaam.

Amesema Brela inaungana na Shirika la Miliki Bunifu Duniani (WIPO) kuadhimisha siku ya miliki bunifu, ambayo huadhimishwa kila mwaka April 26, lakini kutokana na upekee wa siku hiyo kwa Tanzania itaadhimishwa kesho.

Amesema katika maadhimisho hayo kutakuwa na ushiriki wa viongozi mbalimbali, ambao pia watajadili manufaa ya teknolojia na ubunifu nchini.

Isome pia:https://habarileo.co.tz/wp-admin/post.php?post=51558&action=edit

Amesema kaulimbiu ni miliki ubunifu na malengo ya maendeleo endelevu katika kujenga mustakabali wa pamoja kwa kutumia ubunifu.

Mhando amesema lengo la kauli mbiu hiyo ni kutambua umuhimu wa miliki bunifu na mchango wake katika maendeleo endelevu, kwa kuwa bila ubunifu maendeleo ni kazi kuyafikia.

Amesema ubunifu ni chachu ya maendeleo katika nyanja zote, ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) lazima matumizi ya miliki bunifu yafikiwe.

Amesema katika siku hiyo itakuwepo majadiliano mbalimbali yakihusisha utaalam wa kibunifu na maendeleo, namna miliki bunifu inaweza kutumika kuleta maendeleo na namna nchi inavyoweza kutambua mchango wa wabunifu katika kuleta maendeleo.

 

Habari Zifananazo

Back to top button