Uchafu zao la mkonge wageuzwa chakula cha mifugo

MWANAFUNZI  wa Shahada ya Uzamivu wa Sayansi ya Mazingira katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi ya Nelson Mandela, Aziza Konyo,  amebuni uchafu unaozalishwa na zao la mkonge  kuwa chakula cha mifugo.

Akizungumza kwenye maonesho ya wakulima Kanda ya Kaskazini yanayoendelea viwanja vya Themi Njiro mkoani Arusha,  Aziza  amesema tafiti  zilizofanyika zimebaini kuwa  asilimia nne hadi sita ya zao la mkonge ni kamba zile nyeupe, lakini asilimia kubwa iliyobaki ni uchafu.

 

Amesema uchafu mwingi unaozalishwa katika zao la mkonge na unaleta athari za kimazingira na kibinadamu,  hivyo katika kuondoa tatizo hilo wanatumia teknolojia ya nzi chuma yenye uwezo wa kuchakata uchafu.

“Kama unakilo 100 za taka nzi chuma hao wana uwezo wa kuchakata ndani ya siku 10 hadi 14 zikabaki kilo 20 hadi 40,” amesema.

Amesema ndani ya siku hizo watawavuna nzi nchuma hao kwa ajili ya kuwaandaa kwa  chakula cha kuku na samaki na asilimia 2O ya mkonge iliyobaki haitupwi bali itatumika kama mbolea nzuri kwa ajili ya mazao ya mbogamboga zisizo na kemikali.

Habari Zifananazo

11 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button