Uchaguzi MODFA kufanyika Ijumaa

UCHAGUZI wa Chama Cha Soka Wilaya ya Monduli (MODFA) mkoani Arusha unatarajiwa kufanyika ijumaa Oktoba 20 mwaka huu katika ukumbi wa Emanyata wilayani humo.

Akizungumza kwa njia ya simu Mwenyekiti wa MODFA, Abedi  Adamu Mushi alisema kuwa awali uchaguzi huo ulikuwa ufanyika jumapili octoba 15 mwaka huu lakini haukafanyika kwa sababu baadhi ya taratibu zilikuwa hazijakamilika.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa wagombea wote waliochukua fomu na kurudisha na majina yao kupitishwa katika usaili wataruhusiwa kugombea.

Mushi alisema na kuvitaka vilabu vyote vilivyosajiliwa katika wilaya Monduli kujitokeza na kushiriki uchaguzi huo lengo ni kutaka kuweka viongozi wenye maono ya kuendeleza soka katika Wilaya ya Monduli.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa hakutakuwa na ujanja ujanja wa kuibuka timu zisizo sajiliwa kwani wahusika watachukuliwa hatua kali kwani siku hiyo kutakuwa na ulinzi mkali dhidi ya wale wenye nia ovu dhidi ya uchaguzi huo.

Alisema Kamati ya Uchaguzi ilishafanya kazi yake na sasa kazi iliyobaki ni ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa MODFA kuchagua viongozi wa kuongoza chama hicho.

Wakati huo Uchaguzi wa Chama Cha Soka Wilaya ya Arumeru (ADFA) unatarajiwa kufanyika octoba 29 mwaka huu katika mji wa Tengeru Wilayani humo.

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka ADFA zilisema kuwa uchukuaji fomu wa kuwania nafasi mbalimbali unaendelea na mwisho wa kuchukua na kurudisha ni oktoba 18 mwaka huu.

Habari Zifananazo

Back to top button