Uchunguzi tuhuma za Gekul waendelea

MANYARA: MWENYEKITI wa Tume ya haki za Binadamu Jaji Mstaafu, Mathew Mwaimu amefika mkoani Manyara, ili kufanya uchunguzi wa tuhuma zinazo mkabili aliyekuwa Naibu Waziri Wa Katiba na Sheria ambaye kwasasa ni Mbunge wa Babati mjini Pauline Gekul.

Aidha Jaji Mwaimu amesema lengo la tume hiyo ni kubaini ukweli juu ya tuhuma zinazomkabili kiongozi huyo.

Kwa upande wake Kamanda wa polisi mkoani Manyara, ACP. George Katabazi akizungumzia siku ya jana ofisi yake imetoa ushirikiano kwa tume hiyo juu ya tuhuma za Mbunge Gekul katika tuhuma za kufanya uzalilishaji kwa kijana Hashimu na Omary na mwenzake.

Tayari jeshi hilo la Polisi limemhoji Gekul kwa tuhuma hizo za kumfanyia ukatili mfanyakazi ambaye amedai aliingizwa chupa kwenye sehemu za siri akidaiwa kutaka kumuua.

Gekul anadaiwa kumfanyia ukatili mfanyakazi wake huyo kwa kile kinachodaiwa kuwa alikwenda hotelini kwake kimkakati.

Sakata hilo liliibuka baada ya video kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii nchini Tanzania, ikimuonyesha Hashimu akieleza jinsi alivyofanyiwa ukatili huo na Gekul ambaye hadi majuzi alikuwa ni Naibu Waziri wa katiba na Sheria kabla ya kuondolewa na Rais Samia Suluhu Hassan Jumamosi usiku ingawa sababu za kutumbuliwa kwake hazikuwekwa bayana.

Habari Zifananazo

Back to top button