Uchunguzi waanza mlipuko kiwanda cha sukari Morogoro

JESHI la Polisi mkoani Morogoro limeanzisha uchunguzi wa kitaalamu kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama ili kujua asili ya ajali ya mlipuko mkubwa uliotokea kwenye moja ya makontena ya kuhifadhia vifaa vya kilimo na ufundi ya Kiwanda cha Sukari Mtibwa na kusababisha vifo vya watu wawili .

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Alex Mkama asema hayo Aprili 15, 2023 wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu tukio hilo ambalo lilitokea Aprili 12, mwaka huu majira ya mchana katika mashamba ya Miwa , eneo la Loliondo , wilaya ya Mvomero , mkoani Morogoro

Watu hao walifariki wakiwa kwenye shughuli zao za kawaida za uchomeleaji wa vyuma ( Welding) kwa kutumia mitungi ya gesi wakati wakiwa wanaandaa paa la kutengeneza kivuli katika enei lao la kazi na ghafla ulitokea mlipuko kutoka katika kontena walilokuwa wakifanyia kazi na kusababisha vifo vyao.

Advertisement

Kamanda wa Polisi wa mkoa huyo amesema kuwa wakati mlipuko huo unatokea , shughuli za upakiaji wa sukari kwenye magari ya kubeba mizingo zilikuwa zinaendelea jirani na eneo ambako mlipuko ulitokea.

Mkama amesema ,mlipuko huo ulisababisha baadhi ya wafanyakazi wa eneo hilo kupata mshituko na majereha katika sehemu mbalimbai za miili yao .

Amesema kuwa waliopoteza maisha wametambuliwa majina yao ambao ni Hamis Said Hamis (29) fundi wa kuchomelea na mfanyakazi wa kiwanda cha Mtibwa na mingine ni Frank Kennedy (26) fundi wa kuchomelea na pia ni mfanyakazi wa kiwanda hicho.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huyo amesema watu wengine 11 wanaendelea na matibabu ya majeraha katika hospitali ya Kiwanda hicho na wengine walitibiwa na kuruhusiwa .

Mkama amesema baada ya kujiridhisha na hali ya usalama kwa sasa, kazi za shamba zinaendelea kama kawaida na huku akitoa wito kwa wafanyakazi wote maeneo ya viwandani kuchukua tahadhari pindi wawapo kazini.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *