UCSAF, kujenga minara ya simu

DAR ES SALAAM: MFUKO wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imeingia mkataba na kampuni mbalimbali ya simu lengo ni kufikisha huduma hiyo katika vijiji 5,111.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Justina Mashiba akizungumza leo Novemba 21, 2023 katika mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar Es Salam amesema mfuko huo utajenga minara 2, 149 ambapo wananchi takribani milioni 23 watapata huduma hiyo ya mawasiliano kwa uhakika.

Amesema wamepeleka vifaa vya Tehama katika shule 1120, pamoja na kufanikisha mradi wa kutoa mafunzo kwa walimu 3139, huku wakitekeleza mradi mwingine wa tiba mtandao utakaowezesha hospitali kutoa huduma za matibabu kwa njia ya mtandao.

Advertisement

Pia amesema, UCSAF imepanga kujenga mnara kila Halmashauri ili kuwa na redio jamii.

Akizunguza kwa niaba ya Wahariri Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Deodatus Balile amepongeza shughuli zinazofanywa na UCSAF na ameshauri kuangaliwa upya kwa gharama zinazotumika za kurusha matangazo kwa njia ya mnara kutokana na gharama hizo kuwa kubwa.

Mfuko wa Mawasiliano kwa wote UCSAF ulianzishwa rasmi mwaka 2009, kwa lengo la kuhakikisha huduma za mawasiliano zinafika Vijijini na mijini pasipokuwa na shida yeyote

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *