Udhibiti wachukuliwa kumwagika kwa ‘Sulphur dioxide’ Morogoro

Wataalamu kutokaTaasisi za serikali katika wapo katika jitihada kubwa ya kudhibiti madhara kwa binadamu na wanyama kufuatia mabehewa 22 yaliyobeba tani 1,099 za kemikali aina ya Sulphur Dioxide na Treni ya mizigo ya Shirika la Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kuanguka mkoani Morogoro.

Treni hiyo ilikuwa inatoka Dar  es Salaam  kuelekea nchini Zambia ikiwa na shehena hiyo na kupata ajali eneo la Lumumwe , lililopo katika halmashauri ya Mlimba ,wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

Mkuu wa kitengo cha Usalama Shirika la Reli Tazara nchini Tanzania anayesimamia Kituo cha Mlimba Amani Mboliko amesema ajali hiyo imetokea Novemba 30,2022 .

Amesema ajali hiyo imetokea baada ya hitilafu katika mfumo wa breki ,na hivyo injini ilishindwa kuvuta behewa zote na kuifanya irudi nyuma kwa zaidi ya kilometa nane na kusababisha yote kuanguka.

Naye Meneja Ofisi ya Mkemia mkuu wa serikali kanda ya kati, Gerald Merinyo anasema tayari jitihada za kuhakikisha kemikali yote iliyomwagika inaondolewa zinaendelea kufanyika kupitia wataalamu mbalimbali.

Amesema licha ya kuchukuliwa kwa tahadhari hiyo ametoa wito kwa taasisi zote zinazojiusisha na usafirishaji wa kemikali kuhakikisha zinatoa mafunzo ya kutosha kwa wafanyakazi ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza .

Naye mkaguzi msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji , Mohamed Madulika amesema zoezi linaendelea ili kuhakikisha mabehewa yote yanaondolewa eneo la ajali bila ya kuleta madhara kwa binadamu na viumbe hai vingine.

Kwa upande wao Meneja wa utekelezaji wa sheria kutoka kurugenzi ya utekelezaji wa sheria Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Jamali Baruti pamoja na kaimu Meneja wa baraza hilo kanda ya Morogoro Rufiji , Mhandisi Jane Kadoda kwa nyakati tofauti wametaja madhara yatokanayo na kemikali hiyo kwa wanayama na binadamu.

Kwa mujibu wa wataalamu hao wa NEMC kuwa madhara kwa wanyama wanaweza kufa endapo sumu hiyo itatiririka mpaka kwenye vyanzo vya maji.

Kwa upande wa binadamu , kemikali hiyo inapowaka moto inatoa halufu na inaweza kusababisha kifo, mwili kuwasha na macho kuwa mekundu.

Habari Zifananazo

Back to top button