Udokozi wa vifaa vya ujenzi uachwe

RAIS  Samia Suluhu Hassan ameagiza wakandarasi pamoja na wafanyakazi katika miradi mbalimbali nchini kusimamia vifaa vya kazi ili kuepusha wizi unaofanywa na wafanyakazi ambao sio waaminifu ili kuepuka gharama ambazo sio za lazima.

Amesema miradi hiyo imekuwa ni chanzo kizuri cha ajira kwa Watanzania hivyo wanatakiwa kutumia nafasi hiyo kupata fedha halali za kuendesha familia zao.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania Mohammed Besta alisema Daraja la Johm Magufuli Kigongo Busisi lina urefu wa kilomita tatu na barabara unganishi yenye urefu wa kilomita moja, linatarajiwa kutumia sh bilioni 716.33

Habari Zifananazo

Back to top button