UDSM kuongeza masomo kwa wenye uhitaji

UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (CKD) umesema kuwa utaongeza fursa za masomo kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum ili waweze kufikia malengo na kutimiza ndoto zao.

Hayo yalisemwa jana na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa William Anangisye ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

“Nakipongeza kituo cha huduma cha watu wenye mahitaji maalum katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa kuona umuhimu wa kuandaa maadhimisho ya watu wenye ulemavu mwaka 2023 hapa chuoni.

Advertisement

“Jambo hili linaongeza uelewa kwa jamii kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na elimu bora na ajira vile vile nakipongeza kituo hiki kwa kuandaa ripoti ya mwelekeo kwa usaili wa wanafunzi wenye mahitaji maalum kutoka mwaka 1978 hadi 2023,” alisema Profesa Anangisye.

Alisema ripoti inaonyesha jinsi usajili ulivyoongezeka kwa kipindi cha miaka 45, wanafunzi wamesajiliwa kwa mahitaji maalum waliyonayo, jinsi zao , kiwango cha elimu na ndaki au shule kuu wanazotokea.

“Ripoti hii itatusaidia katika kufanya maamuzi mbalimbali kuhusu vifaa vinavyohitajika wataalamu na maboresho kulingana na aina ya wanafunzi wenye mahitaji maalum tunaowahudumia.

“Nimefurahi kusikia kwamba tangu mwaka wa masomo 1978/79, hadi sasa mwaka 2022/23 takwimu zinaonyesha kwamba chuo chetu kimefanikiwa kutoa huduma za kielimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum takribani 621, katika nyanja mbalimbali za mafunzo.

“Kati ya hao 457 wamekwisha hitimu na 164 wanaendelea na masomo yao ningependa niongelee takwimu za wanafunzi waliopo inaonyesha kati ya wanafunzi 164 wanaochukua masomo ya uzamili na uzamivu ni 19 sio namba nzuri lakini inatosha,” alisema Profesa Anangisye.

Alisema takwimu hizi zinawataka kutafuta mbinu mbalimbali za kuongeza fursa za masomo ya uzamili na uzamivu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum ili waweze kuifanyia kazi kauli mbiu ya watu wenye mahitaji maalum katika kufikia malengo na maendeleo endelevu kwa kila binadamu na kila mtanzania bila kujali ana hali gani.

“Hivyo ni jukumu letu kama viongozi kukumbushana katika kuhakikisha wenzetu wanafikia haya maana yake nini kuongeza idadi yao kwenye digrii zao kwenye uzamili na uzamivu wanapohitimu wanatengeneza mazingira mazuri.

“Naomba nitumie maadhimisho haya kuweka mkazo zaidi kwa kutoa huduma bora kwa watu wenye mahitaji maalum kwa kutambua elimu ni nyenzo maalum kwenye maisha ya kila mtanzania vilevile nitumie fursa hii kuwahimiza wanafunzi wanaochukua shahada za uzamili na uzamivu kujitahidi kumaliza masomo yenu kwa wakati ili kituo kitoe nafasi kwa watu wengine,” alisisitiza Profesa Anangisye.

Alisema hadi sasa chuo kinasomesha wanafunzi watano lakini mipango yao ni kuongeza namba kusomesha kwa upande wa Masters na PHD.

“Naomba nitoe angalizo hatutatoa msaada huo wa masomo kwasababu tu mtu ana ulemavu maalum tutatoa ikiwa na uwezo wa kitaaluma hii inawezekana.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *