UDSM wazindua kigoda cha taaluma utafiti wa uhamiaji

CHUO Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) kimezindua Kigoda Cha Utafiti wa Kitaaluma wa Uhamiaji usio wa halali,  ili  kuangazia sababu za uhamiaji huo namna ya kuwahudumia na namna ya kuepuka uhamiaji usio halali.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo ambao umefanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam, Kaimu Makamu wa chuo upande wa Taaluma Prof.Boniventure Rutinwa amesema utafiti utafanyika katika mazingira ya kawaida pamoja na kutoa elimu kwa watu kwa kutoa machapisho pamoja na kufanya semina mbalimbali.

Amesema kuwa vita, uharibifu wa mazingira na miradi ya maendeleo ni kati ya vitu vinavyoweza kusababisha uhamiaji usio wa halali.

Kwa upande wake Msimamizi wa Utafiti, Opportune Kweka amesema utafiti utahusisha washiriki 32 kutoka mataifa mbalimbali na vilevile utafiti huo unagusa utu wa wakimbizi hususan katika kupata kwao mahitaji muhimu.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x