DOLA milioni 100 zinatumika kwenye uchimbaji mkubwa wa madini huku Dola milioni 10 mpaka Dola milioni 99 ni uchimbaji wa kati Dola milioni 9 ni uchimbaji mdogo.
Hayo ameyasema Waziri wa Madini, Dk Doto Biteko wakati akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya mkutano wa madini utakaofanyika tarehe 25-26 Oktoba mwaka huu katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Madini Nchini, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maji, Nishati na Madini Zanziber pamoja na wadau wa madini.
Waziri Biteko amesema Mkutano huo utakuza sekta ya Madini na kufungamanisha sekta hiyo na Sekta ya Utalii
Aidha ameongezea kuwa Asilimia 40% ya wauzaji wa madini imetokana na Wachimbaji wadogo wa madini Nchini….Cue…
Kwa upande wake katibu Mkuu Wizara ya Maji Nishati na Madini, Joseph Kilanga amesema mkutano utaongeza watalii na kuongeza ushirikiano baina ya Tanzania na Zanziber…Cue…
Aidha muaandaji wa Mkutano huo Abdusamad Abdulrahim amesema Mkutano huo utaleta wawekezaji zaidi ya elfu mbili kutoka Nchi za Nje pamoja na kanda zote za Afrika.