Ufaransa kuondoa ubalozi, wanajeshi Niger

RAIS wa Ufaransa, Emmanuel Macron amesema nchi yake itauondoa balozi na wanajeshi wake kutoka Niger kufuatia mapinduzi ya Julai yaliyompindua Rais Mohamed Bazoum. Mtandao wa Al-Jazeera umeripoti.

“Ufaransa imeamua kumuondoa balozi wake. Katika saa zijazo balozi wetu na wanadiplomasia kadhaa watarejea Ufaransa,” Macron alisema katika mahojiano na moja ya kituo cha habari Jumapili.

Aliongeza kuwa ushirikiano wa kijeshi “umekwisha” na kwamba wanajeshi 1,500 wa Ufaransa walioko nchini humo wataondoka wiki chache zijazo na watakamilisha dhumuni hilo mwishoni mwa mwaka huu.

Kujiondoa kwa Ufaransa kunakuja baada ya shinikizo kutoka kwa jeshi na   na maandamano ya hivi karibuni katika mji Mkuu Niamey, ikiwa ni pamoja na nje ya kambi ya kijeshi inayohifadhi wanajeshi wa Ufaransa.

Watawala wapya wa Niger, ambao walikuwa wakitaka Ufaransa iondoke baada ya Macron kukataa kuyatambua mapinduzi ya Julai 26, walikaribisha tangazo la Rais wa Ufaransa.

​”Jumapili hii, (Jana) tunasherehekea hatua mpya kuelekea uhuru wa Niger,” walisema katika taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa. “Huu ni wakati wa kihistoria, ambao unazungumzia dhamira na mapenzi ya watu wa Niger,” waliongeza.

Haya yanajiri wakati wanajeshi wa Ufaransa pia wakitakiwa kuondoka katika makoloni yake ya zamani Mali na Burkina Faso.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Juliaropst
Juliaropst
2 months ago

Single Mom With 4 Kids Lost Her Job But Was Able To Stay On Top By Banking Continuously DOLLER 1500 Per Week With An Online Work She Found Over The Internet… 

Check The Details HERE…..  https://smartcareer12.blogspot.com/

Last edited 2 months ago by Juliaropst
money
money
2 months ago

Mashindano ya nani kuhinda kwenye neno “ABROAD“ NCHINI TANZANIA!?

MJERUMANI

MHINDI

MTANZANIA

MKENYA

MNIGERIA

MHISPANIA

file:///C:/Users/User/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image002.jpg

NANI AINGIZE NDEGE ZA KWENDA KUMSALIMIA BABU NA BIBI, KWA ALIYESHINDA KULELEWA NA BIBI TU!?

Capture.JPG
Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x