Ufaransa yaipa tano serikali miradi ya maji

UFARANSA: Serikali ya Ufaransa imesema inatambua na kuthamini jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan katika dhamira ya kuimarisha huduma ya maji kwa wananchi.

Waziri wa Nchi, Maendeleo ya Uchumi wa Ufaransa, Chrysoula Zacharopoulou akizungumza na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema, Ufaransa inaamini huduma ya maji ni miongoni mwa vipaumbele vyake katika kipindi cha uongozi wake.

Amesema, katika kuunga mkono jitihada hizo serikali yake ya awamu ya sita na Serikali ya Ufaransa imejipanga kuwekeza katika miradi mingi ya maji zaidi kwa kuthamini kazi anayoifanya na pia umuhimu wa sekta kwa maisha ya watu kwani maji ni uhai.

Pia, Kiongozi huyo ameipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Samia kwa serikali yake kukamilisha miradi ya maji mikubwa na ya kimkakati na usimamizi mzuri wenye kujali thamani ya fedha ikiwemo miradi ya mashirikiano inatekelezwa kati ya Tanzania na Ufaransa kupitia Shirika la Maendeleo Ufaransa AFD kama Miradi ya maji miji ya Shinyanga, Musoma, Bukoba, Mwanza, Morogoro na mradi wa Majitaka eneo la Kurasini Jijini Dar es Salaam.

Nae, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amewasilisha salamu za shukrani za Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji uliofanyika katika sekta ya maji na kushukuru kwa serikali ya Ufaransa kuridhia mapendekezo ambayo Rais alimuagiza kuwasilisha ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa mradi wa maji chanzo cha Ziwa Victoria Jijini Mwanza awamu ya pili ya usambazaji maji baada ya ujenzi wa miundombinu kukamilika.

Habari Zifananazo

Back to top button