Waziri Mkuu mdogo zaidi ateuliwa Ufaransa

RAIS wa Ufaransa, Emmanuel Macron jana alimteua Gabriel Attal kuwa Waziri Mkuu mpya, na hivyo kumfanya kuwa Waziri Mkuu wa kwanza kijana (34) katika historia ya taifa hilo.

Attal anachukua nafasi ya Élisabeth Borne, ambaye alijiuzulu Jumatatu baada ya kuhudumu kwa miezi 20, imeripotiwa kuwa hatua ya Macron inalenga kuunda serikali mpya.

Akiwa na umri wa miaka 34, ndiye Waziri Mkuu mdogo zaidi katika historia ya Ufaransa, akimzidi cheo Msoshalisti Laurent Fabius aliyekuwa na umri wa miaka 37 alipoteuliwa na François Mitterrand mwaka wa 1984.

Attal, ambaye kwa sasa ni Waziri wa Elimu, atakuwa na jukumu la kuiongoza Serikali ya Ufaransa katika uchaguzi muhimu wa Bunge la Ulaya mwezi Juni.

Habari Zifananazo

Back to top button