‘Ufugaji utanyanyua ajira kwa vijana, wanawake’

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema ufugaji wa viumbe vya majini na mifugo mingine ndio utakaonyanyua ajira ya vijana na wanawake hapa nchini.

Amesema hayo katika kilele cha madhimisho ya Nanenane  jijini Mbeya baada ya kutembelea banda la uvuvi llililopo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

” Tuna madini tutachimba yataisha. Tuna mambo mengine yatakuja yataondoka, lakini ardhi na maji aliyotupa Mungu yapo inabidi tuyatumie na hii ndio maana ya uchumi wa buluu katika kujenga nchi yetu,” amesema.

Awali ameishukuru wizara kwa kuwa imechangamka na Program ya Kielelezo, ” Jenga Kesho iliyo Bora” BBT-LIFE kwa vijana wameingia kwenye kufuga sana samaki na vifaa vingine.

” Nimefurahi sana vijana. Jitihada hizi serikali imetumia pesa nyingi sana. Bajeti ya mwaka jana na mwaka huu pesa nyingi sana imeenda kilimo.

“Mama yenu nazunguka ulimwenguni natafuta pesa kwa ajili yenu. Nje ya bajeti ya serikali nikijua kwamba kupitia kilimo cha mazao, ufugaji wa samaki, ufugaji wa nyuki misitu lakini pia kilimo cha mazao ya aina zote.

” Hayo ndio yatanyanyua ajira ya vijana lakini na wanawake,” amesema.

Awali kijana mnufaika wa BBT, Michael Biliba amesema vijana 200 wamenufaika na program hiyo kwa kuwa wamepata elimu kwa vitendo kuhusiana na elimu ya viumbe wa maji chumvi na maji baridi.

” Viumbe wa maji chumvi kule tumejifunza zaidi namna ya kunenepesha kaa. Kaa ni viumbe wako hatarini kupotea kwa sababu wana thamani sana na wanahitajika sana,” amesema.

Amesema hapa nchini kilo moja ni kati ya sh 5000 hadi 10,000, wakisafirishwa nje wanaanzia Sh 20,000 hadi Sh 50,000.

Amesema pia wamejifunza kilimo cha mwani ambacho soko la ndani ni kuanzia Sh 1 700 hadi Sh 2,300, ikisafirishwa nje ni Sh 5000 na kuendelea kwa kilo.

Pia amesema wamejfunza kuhusu majongoo bahari ambayo soko la ndani kilo ni Sh 150,000 mpaka Sh 200,000 lakini soko la nje kilo moja ni kuanzia Sh 900,000.

Awali Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema walipata Sh bilioni 26  ambazo zilitengeneza vizimba 600 na kununua boti 160 za kisasa.

” Cage unayoiona imetengenezwa na vijana. Na lengo lake kubwa ni kongeza uzalishaji wa samaki aina ya sato.

“Tutakapofanikiwa kuwa na uzalishaji mkubwa wa sato, maana yake tutaondoa pengo kati ya uzalishaji wa tani 400,000 na mahitaji ya tani 700,000,” amesema.

Amesema wanaongeza uzalishaji wa sato kwa kuwa Watanzania wengi wanapenda aina hiyo ya samaki ili kumfanya sangara aende viwandani kisha kusafirishwa nje ya nchi.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Melissaoward
Melissaoward
4 months ago

Single Mom With 4 Kids Lost Her Job But Was Able To Stay On Top By Banking Continuously DOLLER 1500 Per Week With An Online Work She Found Over The Internet… 

Check The Details HERE…..  https://webonline76.blogspot.com/

Last edited 4 months ago by Melissaoward
Julia
Julia
3 months ago

Earn income while simply working online. Work from home whenever you want. Just for maximum 5 hours a day you can make more than $600 per day online. From this I made $18,000 last month in my spare time.
.
.
Detail Here———————————————>>>  http://Www.OnlineCash1.Com

services@tra.go.tz
services@tra.go.tz
3 months ago

habari leo

MAPINDUZI HALISI.PNG
services@tra.go.tz
services@tra.go.tz
3 months ago

habari leo DAIMA

MAPINDUZI.jpg
services@tra.go.tz
services@tra.go.tz
3 months ago

ZIMBABWE

MAPINDUZI HALISI.PNG
Back to top button
5
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x