Uganda kupitia upya sera ya wakimbizi

SERIKALI ya Uganda, imesema huenda ikalazimika kupitia upya sera yake ya kuwapa hifadhi wakimbizi, ikiwa jumuiya ya kimataifa itaendelea kusalia kimya katika kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na ongezeko la wakimbizi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Misaada na Kukabiliana na Majanga, Hilary Onek ambapo amesema nchi yake inahangaika kupata zaidi ya Dola bilioni 1 zinazohitajika kwa mwaka ili kuwahudumia wakimbizi.

Onek amesema kama hali itaendelea kuwa mbaya na hawatapata fedha hizo kwa wakati, basi hawatakuwa na namna zaidi ya kupitia upya sera yake kuhusu wakimbizi.

Aidha Onek amesema sera yake ya sasa inawagharimu, na kwamba wakati umefika kwa jumuiya ya kimataifa kuingilia kati kuisaidia nchi yake ili iweze kuhudumia idad kubwa ya wakimbizi wanaoendelea kuwasili nchini humo.

Kwa sasa nchi ya Uganda, inatoa hifadhi kwa wakimbizi zaidi ya milioni moja huku ikitaja idadi kubwa ya wakimbizi ambao huingia nchini humo wakitokea DR Congo, Sudan Kusin na Somalia.

Habari Zifananazo

Back to top button