MAMLAKA ya afya Uganda inachunguza mlipuko wa ugonjwa ambao haujatambulika hadi sasa uliouwa watu 12 kwa wiki mbili katika Wilaya ya Kyotera.
Imeelezwa waathirika walianza kuwa na vipele ambavyo muda unavyozidi kwenda vinakuwa vikubwa, huku wengine wakivimba miguu na mikono.
Wizara ya Afya imekusanya sampuli mpya za ngozi kutoka kwa mmoja wa wagonjwa waliofariki katika hospitali kuu ya eneo hilo.
Aidha matokeo hayatolewa hadharani bado. Maofisa afya wanasema baadhi ya wagonjwa walikimbilia kwa waganga wa kienyeji badala ya vituo vya afya.
–
Wamesema imekuwa vigumu kuwazuia kwa kuwa ugonjwa bado haujajulikana.