SERIKALI ya Uganda imetenga $800m kukuza na kufundisha lugha ya Kiswahili nchini humo, kama sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano wa kikanda.
Watumishi wa umma wakiwemo madaktari, wauguzi na wafanyakazi wa mpakani watapewa kipaumbele katika programu ya mafunzo ya Kiswahili ambayo bado haijazinduliwa, Waziri wa Uganda wa Masuala ya Afrika Mashariki Rebecca Kadaga alisema.
Waziri hakutoa maelezo zaidi kuhusu lini na jinsi gani programu ya mafunzo itazinduliwa.
Ikiwa ni sehemu ya juhudi za kueneza lugha hiyo nchini humo, Kadaga alisema viongozi wote waandamizi wa serikali wakiwemo mawaziri na majaji wanasoma masomo ya lazima kila wiki.