Ugonjwa wa shinikizwa la damu waongezeka kwa 95%

UGONJWA wa shinikizo la juu la damu umeongezeka kutoka wagonjwa 688,901 kwa mwaka 2017 hadi kufikia wagonjwa 1,345,847 kwa mwaka 2021 sawa na ongezeko la asilimia 95.4 katika kipindi cha miaka mitano.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameyasema hayo leo Mei 17,2023 ikiwa ni siku ya Maadhimisho ya shinikizo la damu duniani

“Takwimu hizi zinatuonesha kwamba wagonjwa hawa wenye shinikizo la damu wameonekana kuongezeka takribani mara mbili zaidi kwa kipindi cha miaka mitano.” Amesema Ummy

Amesema kwa ujumla magonjwa yasiyoambukizwa yameongezeka kwa asilimia 9.4 kwa kipindi cha miaka mitano kutoka mwaka 2017 hadi mwaka 2021 kwenye vituo vya Afya chini, wagonjwa hawa wameongezeka hadi kufikia wagonjwa 3,440,708 kwa mwaka 2021.

Pia, amesema takwimu zinaonyesha watu watatu hadi wanne kati ya 10 wana shinikizo la juu la damu kwa uchunguzi uliofanywa katika jamii kwenye mikoa ya Pwani, Arusha, Geita, Mtwara, Lindi, Zanzibar, Iringa na Dares Salaam.

Kwa upande wa dawa, Ummy amesema Wizara imeruhusu dawa za kukabili shinikizo la juu la damu katika ngazi ya msingi kwa kuruhusu dawa tatu, ambazo ni Losartan, Amlodipine na Hydralazine kutumika katika ngazi ya kituo cha afya na dawa mbili ambazo ni Nifedipine na Frusemide ambazo hutumika katika ngazi ya zahanati.

Amesema, mpango wa serikali kupitia Wizara ya Afya ni kutoa mafunzo ya utoaji wa huduma za magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo huduma za ugonjwa wa shinikizo la damu kwa watoa huduma 2400 kutoka vituo vya Afya vyote 600 katika mikoa yote 26.

Aidha,Ummy amewakumbusha Watanzania juu ya umuhimu wa kubadili mtindo wa maisha kwa kuzingatia ufanyaji wa mazoezi, kuepuka tabia bwete, kuepuka matumizi ya tumbaku na bidhaa zake na kupunguza matumizi ya vilevi.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x