Ugonjwa wa Sukari, UTI, minyoo yatikisa 2023

UGONJWA wa sukari, shinikizo la juu la damu, mfumo wa hewa, UTI na ugonjwa kuharisha ni miongoni mwa magonjwa 10 yaliyosumbua wananchi wengi nchini kwa mwaka 2023.

Akizungumza leo Januari 10, 2023 jijini Dar es Salaam, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema magonjwa hayo bado yapo juu na ni tishio nchini.

Ummy amesema takribani watu watu 6,52,455 sawa na  asilimia 2.5 yaligundulika kuwa na ugonjwa wa sukari katika mwaka 2023.

“Zamani miaka kama mitatu nyuma tulikuwa hatuoni kisukari wala shinikizo la juu la damu katika magonjwa 10 yaliyokuwa yakiongoza katika wagonjwa wa nje nchini, tutaeleza ni lipi ambalo tumejipanga kufanya,”amesema Ummy

Amesema, kwa upande wa watoto chini ya umri wa miaka mitano maambukizi ya mafua na kikohozi ni asilimia 38.8.

“Kwa hiyo katika kila watoto 100 mwaka 2023 waliokwenda kwenye Vituo vya kutoa huduma za afya watoto takribani 39 walikwenda kwa sababu au waligundulika maambukizi katika mfumo wa hewa wa juu, malaria nayo imekuja juu kwa asilimia 10.7.” amesema Ummy na kuongeza

“Ugonjwa wa kuharisha bila upungufu wa maji ni asilimia 8.4, maambukizi kwa njia ya mkojo asilimia 7.5, Homa ya Mapafu/Nimonia asilimia 7.4, maambukizi ya ngozi asilimia 3.8, magonjwa mengineyo ya mfumo wa chakula, magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza asilimia 3.8.

Amesema  minyoo kwa watoto nayo imeingia ikiwa na asilimia 2.9, kuharisha na upungufu wa maji asilimia 2.3 na maambukizi ya ngozi au fangas asilimia 2.2.

“Kwa hiyo kama tunazungumzia matibabu kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano picha inayotupa ni kwamba asilimia takriabi 55 ya watoto wetu wanaumwa Malaria na kuharisha bila upungufu wa maji,” amesema Ummy ”

Amesema hiyo inaisaidia serikali kutambua aina ya dawa ambazo zinapaswa kuwa katika vituo vya afya, zahanati na hospitali kwa saa 24 kwa miezi yote 12.

Aidha, amesema kwa upande wa watu wazima, magonjwa yaliyotikisa kwa mwaka 2023 ni maambukizi katika mfumo wa hewa wa juu kwa asilimia 18.9 kati ya Watanzania 100 ambao walikwenda Hospitali Watanzania 19 walikuwa au walikutwa na maambukizi katika mfumo wa hewa wa juu, asilimia 15.8 maambukizi katika njia ya mkojo (UTI) kati ya watu 100 waliokwenda Hospitali watu 16 walikutwa na UTI saw ana asilimia 15.8.

Malaria imechomoza pia kwa watu wazima asilimia  kwa asilimia 6.9, shinikizo la juu la damu asilimia 5.6, Vidonda vya tumbo vinaongezeka kwa  asilimia 3.7.

Habari Zifananazo

Back to top button