DAR ES SALAAM; Indonesia na Tanzania zimesherehekea historia ya uhusiano wa mataifa hayo mawili katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam.
Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Tri Yogo Jatmiko, amesema mataifa hayo licha ya kuwa mbali kijiografia na kusababisha changamoto za kibiashara, lakini zina ukaribu mkubwa wa mila, tamaduni na maadili.
Pia amesema serikali hizo mbili zina mpango wa kukaa kujadili njia za kuboresha sekta ya usafirishaji na changamoto zinazozikabili nchi hizo mbili.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Mizara ya Mambo ya Nje, Balozi Samwel Shelukindo ameeleza Tanzania wanaweza kupata masoko ya biashara kupitia uwekezaji wa nchi mbalimbali ikiwemo Indonesia na kuahidi kuendeleza uhusiano huo uliodumu kwa takribani miaka 60.
Pia mwekezaji kutoka Indonesia Feri Augustine, amesema ana imani uhusiano uliopo baina ya Tanzania na Indonesia una nguvu kubwa katika maendeleo na utaendelea kudumu.