Uingereza hawana haraka kutuma vikosi Ukraine

UINGEREZA imesema hakuna mipango ya haraka ya kupeleka vikosi vya kijeshi nchini Ukraine, Waziri Mkuu, Rishi Sunak amesema.

Hatua hiyo ni baada ya waziri wake wa ulinzi kupendekeza kuwa wanajeshi wanaweza kufanya mafunzo nchini humo.


Hadi sasa, Uingereza na washirika wake wamesitisha kupelekea vikosi vya kijeshi Ukraine ili kupunguza hatari ya mzozo na Urusi.


Waziri wa Ulinzi wa Uingereza, Grant Shapps ambaye aliteuliwa kushika nafasi hiyo mwezi uliopita, alisema katika mahojiano na Gazeti la The Sunday Telegraph kwamba anataka kupeleka wakufunzi wa kijeshi nchini Ukraine, pamoja na kutoa mafunzo kwa vikosi vya kijeshi vya Ukraine au nchi nyingine za Magharibi.



Saa chache baada ya mahojiano hayo kuchapishwa, Sunak alisema hakuna mipango ya haraka ya kutuma wanajeshi wa Uingereza nchini Ukraine.

” Waziri wa ulinzi alichokisema ni kwamba huenda ikawezekana siku moja katika siku zijazo kwa sisi kufanya baadhi ya mafunzo hayo nchini Ukraine,” Sunak aliwaambia waandishi wa habari mwanzoni mwa kongamano la kila mwaka la chama tawala cha Conservative mjini Manchester.

“Lakini hilo ni jambo la muda mrefu, si la hapa na pale. Hakuna wanajeshi wa Uingereza ambao watatumwa kupigana katika mzozo uliopo.”aliongeza Sunak.

Habari Zifananazo

Back to top button