Uingereza kutangaza Wagner kundi la kigaidi

LONDONUingereza inakusudia kulitangaza kundi la mamluki la Wagner la nchini Urusi kuwa shirika la kigaidi lililopigwa marufuku, ikisema kuwa bado ni tishio kwa usalama wa kimataifa hata baada ya kifo cha kiongozi Yevgeny Prigozhin.

Serikali nchini humo imeeleza itapeleka bungeni ‘House of Commons’ mjadala wa kuzuia kundi hilo chini ya Sheria ya Ugaidi.

Endapo suala hilo likiidhinishwa na wabunge, utazuia uanachama au uungwaji mkono kwa Wagner, ambao amekuwa na jukumu kubwa la mapigano wakati wa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Pia imefanya kazi nchini Syria na mataifa kadhaa ya Afrika.

Hatua hiyo inayotarajiwa kuanza kutekelezwa ndani ya siku chache, inawajumuisha Wagner katika kundi moja na Islamic State, kundi la wanamgambo wa Palestina Hamas na wanamgambo wa Ireland Kaskazini.

Katibu wa Mambo ya Ndani, Suella Braverman alisema Wagner “amehusika katika uporaji, utesaji na mauaji ya kinyama. Operesheni zake nchini Ukraine, Mashariki ya Kati na Afrika ni tishio kwa usalama wa kimataifa.”

“Hao ni magaidi, wazi na rahisi na agizo hili la marufuku linaweka wazi hilo katika sheria za U.K.,” alisema.

6 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *