Ujenzi barabara Mbezi Juu, Makongo, Wazo waiva
UJENZI wa barabara za Kata ya Mbezi Juu, Makongo, Wazo na Mbezi Beach unatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila katika uzinduzi wa Mkongo wa Mawasiliano wa Baharini (Submarine Cable) wa 2 Afrika na Teknolojia ya Mawasiliano ya Kasi ya 5G ya Airtel iliyofanyika leo Agosti 10, 2023 Mbezi Bechi Tanki Bovu.
Chalamila amesema, mradi huo kwa sasa upo kwenye hatua ya ‘design’ na siku si nyingi watautangaza na ujenzi kuanza.
“Katika wilaya yetu ya Kinondoni tuna kilomita jumla 170 ambazo zitajengwa kwa kiwango cha lami, awamu ya kwanza ni kilometa 48 na zitagharamu dola za Marekani milioni 38,” amesema Chalamila na kuongeza:
“Awamu ya pili ya mradi huu utaanza mwakani mwezi Februari, nakuhakikishia muheshimiwa Rais, mara baada ya kutoa maelekezo ujenzi huu utaanza mara moja,” amesema.