KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Abdalla Shaib Kaim, amesema mradi wa ujenzi wa Barabara ya Mitengo -Hospitali ya Kanda yenye urefu wa kilomita 1 umekidhi vigezo na matumizi ya fedha yapo vizuri.
Amesema hayo leo Jumapili wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi huo kwa kiwango cha lami, utakaogharimu Sh milioni 500 hadi kukamilika.
Akizungumza wakati wa uzinduzi na ukaguzi wa ujenzi wa mradi huo uliopo Manispaa ya Mtwara Mikindani, kiongozi huyo amesema mradi huo umekidhi vigezo kwani matumizi ya fedha yapo vizuri.
Amesema matumizi ya fedha yanaendana na thamani ya mradi kwani umekuwa na ubora na kukidhi vigezo vinavyostahili.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini, Hassan Mtenga amewataka wananchi katika manispaa hiyo kukata bima ya afya, ili waweze kutibiwa vizuri hospitalini hapo pale watakapopata tatizo la kiafya.
Mradi huo wa Barabara unajengwa na Wakala na Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Mtwara, ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 80.