Ujenzi ofisi TMA kanda ya Mashariki wafikia asilimia 25

MRADI wa ujenzi ofisi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Kanda ya Mashariki unaojumuisha kituo cha kutoa tahadhari za Tsunami umefikia asilimia 25.

Mradi huo unaojengwa gharama za Sh bilioni 10 utakamilika Julai 2024.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk Buruhani Nyenzi amekagua maendeleo ya mradi huo unaojengwa maeneo ya Simu 2000 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa ziara yake Dk Nyenzi amesema mamlaka imekuwa wanufaika wakubwa katika uboreshaji wa huduma za hali ya hewa nchini ukiwemo mradi huo ambao utahusika moja kwa moja katika utoaji wa tahadhari za TSUNAMI nchini na hivyo kuongeza tija katika mipango ya nchi.

Aidha Dk Nyenzi amefurahishwa na kasi ya ujenzi unavyoendelea kutokana na hatua mbalimbali ambazo mkandarasi amezichukua ikiwa ni pamoja na kufanya kazi muda wa ziada na kuongeza nguvu kazi ili kuhakikisha makubaliano ya kimkataba yaliyowekwa yanafikiwa kwa wakati.

Dk Nyenzi amesisitiza matumizi ya malighafi zenye ubora na kutoa fursa za ajira kwa wazawa katika mradi huo.

Habari Zifananazo

Back to top button