Ujenzi Soko la Kariakoo tayari kumenoga

DSM; UJENZI wa Soko la Kariakoo lililopo mkoani Dar es Salaam umefikia asiliamia 91, ambapo kiasi cha fedha kilichotumika ni zaidi ya Sh bilioni 16, ambapo kamera zitakazofungwa soko la zamani ni 93 na soko jipya ni 92.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Rehema Madenge amesema hayo alipozungumza na HabariLEO na kueleza kuwa soko hilo litakuwa na uwezo wa kuchukua magari 138 na litakuwa na sehemu za biashara 2662.

“Mpaka Oktoba 5 mwaka huu hatua ya soko lilipofikia ni asilimia 91. Kiasi cha Fedha kilichotumika mkandarasi wa Kampuni ya Estim Construction amelipwa Sh 16,757,972,150.3. Mtaalamu Mshauri amelipwa Sh 876,416,284.51,” amesema.

Ametaja changamoto zilizojitokeza wakati wa ujenzi ni uboreshaji wa michoro ambao umeenda sambamba na utekelezaji wa ujenzi, pamoja na mabadiliko na mahitaji mapya.

Soko Kuu la Kariakoo liliungua Julai 10, 2021 usiku huku wafanyabaishara 224 wakipoteza bidhaa zao. Serikali haikuwaruhusu wafanyabiashara kurudi tena na badala yake ilianza mchakato wa ujenzi wa soko jipya na ukarabati wa jengo la zamani.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
5
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x