Ujenzi soko la Kariakoo wafikia asilimia 75

UJENZI wa soko la Kariakoo umefikia zaidi ya asilimia 75 ukigharimu shilingi bilioni 28.

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, amesema leo Juni 24, 2023 kuwa baada  ya ajali ya moto ya soko umefanyika kazi mbili moja  ya kujenga jengo jipa la ghorofa nne juu  na ghorofa mbili chini.

“Baada ya ajali ya moto soko la Kariakoo tumefanya kazi mbili moja ni kujenga jengo jipya la ghorofa nne juu na ghorofa mbili chini na ujenzi wake umefikia zaidi ya asilimia 75 na pia kufanya ukarabati wa soko la zamani na shilingi bilioni 28 zimetumika kwa ajili ya kazi hiyo.” Amesema Msigwa

Ujenzi wa soko hilo unaojengwa na kampuni ya Estim Construction Ltd umefikia hatua ya kumwaga jamvi la ghorofa ya tano kati ya ghorofa sita ikihusisha ghorofa mbili za chini ya ardhi (basement).

Soko Kuu la Kariakoo liliungua Julai 10, 2021 usiku huku  wafanyabaishara 224 wakipoteza bidhaa zao. Serikali haikuwaruhusu wafanyabiashara kurudi tena na badala yake ilianza mchakato wa ujenzi wa soko jipya na ukarabati wa jengo la zamani.

Ujenzi wa soko hilo unataraijwa kukamilika Oktoba, 2023 na litakapokamilika litakuwa na uwezo wa kuchukua wafanyabiashara 2,300 sawa na ongezeko la wafanyabiashara 638 ukilinganisha na wafanyabiashara 1,662 waliokuwepo kabla ya ukarabati wa jengo la zamani na ujenzi wa jengo jipya

Habari Zifananazo

Back to top button