Ujerumani yachukua udhibiti wa kampuni 3 za mafuta za Urusi

UJERUMANI imechukua udhibiti wa viwanda vitatu vya kusafisha mafuta vinavyomilikiwa na Urusi nchini humo ili kuhakikisha usalama wa nishati kabla ya marufuku ya mafuta kutoka Urusi kuanza kutekelezwa mwaka ujao, maafisa walisema Ijumaa.

Kampuni tanzu mbili za kampuni kubwa ya mafuta ya Urusi Rosneft – Rosneft Deutschland GmbH na RN Refining & Marketing GmbH – zitawekwa chini ya usimamizi wa Wakala wa Mtandao wa Shirikisho la Ujerumani, Wizara ya Uchumi ilisema katika taarifa.

Kutokana na hali hiyo, shirika hilo pia litadhibiti hisa za makampuni katika viwanda vya kusafishia mafuta PCK Schwedt, MiRo na Bayernoil, vilivyoko mashariki na kusini mwa Ujerumani.

“Huu ni uamuzi wa sera ya nishati unaolenga kulinda nchi yetu,” Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alisema. “Tumejua kwa muda mrefu kuwa Urusi sio muuzaji wa kuaminika wa nishati tena.”

“Kwa uamuzi wa leo, tunahakikisha kwamba Ujerumani inapewa mafuta katika muda wa kati na mrefu pia,” Scholz alisema. “Hiyo ni kweli hasa kwa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Schwedt.”

Kituo hicho kinatoa bidhaa za petroli kwa sehemu kubwa ya kaskazini-mashariki mwa Ujerumani, ikiwa ni pamoja na Berlin.

Rosneft inachukua takriban asilimia 12 ya uwezo wa kusafisha mafuta wa Ujerumani, ikiagiza mafuta yenye thamani ya euro milioni mia kadhaa kila mwezi, wizara hiyo ilisema.

Ilisema hatua hiyo itasaidia kuhakikisha usambazaji wa nishati unaendelea na ilipaswa kudumu kwa miezi sita.

Habari Zifananazo

Back to top button