Ujerumani yatoa neno ushirikiano na Tanzania

UJERUMANI: Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani ,Frank Walter Steinmeier amesema Serikali yake itaendelea kuunga mkono jitihada za maendeleo nchini Tanzania zinazotekelezwa na Serikali inayoongozwa na Rais, Samia Suluhu Hassan.
Ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya kupokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani , Hassani Iddi Mwamweta kwenye Ikulu ya Ujerumani Desemba 8, 2023.
Rais Steinmeier alifafanua Tanzania na Ujerumani zinashirikiana kwenye maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa miradi ya afya, elimu, utunzaji wa mazingira, utamaduni, uhifadhi wa mazingira, utalii, biashara, uwekezaji pamoja na kubidhaisha kiswahili.

Itakumbukwa Rais huyo alifanya ziara ya siku tatu nchini Tanzania kuanzia Oktoba 31 hadi Novemba 1,2023 akiwa ameambatana na ujumbe wa Makampuni mbalimbali kwa ajili ya kuangalia fursa ili kuwekeza nchini.

 
Pamoja na ratiba nyingine akiwa nchini alifanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan.

Habari Zifananazo

Back to top button