Ujerumani yawapa Ukraine vifaru vya vita

Taifa la Ujerumani limethibitisha kuwa kuwapa Ukraine vifaru viwili vya ‘Leopard’ vya vita na kuidhinisha maombi ya nchi nyingine kufanya hivyo.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak amesema hatua ya Ujerumani na washirika wengine wa ‘NATO’ kutuma vifaru nchini Ukraine ni uamuzi sahihi.

Picha na Al-Jazeera

“Uamuzi sahihi wa Washirika wa NATO na marafiki kutuma mizinga ya vita Ukraine, utaimarisha nguvu ya ulinzi Ukraine. Kwa pamoja, tunaharakisha juhudi zetu kuhakikisha Ukraine inashinda vita hivi na kupata amani ya kudumu,” Sunak aliandika kwenye Twitter.

Waziri Mkuu wa Poland, Mateusz Morawiecki amemshukuru Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz kwa uamuzi wa kutuma mizinga miwili ya Leopard nchini Ukraine.
“Uamuzi wa kutuma Leopards kwa Ukraine ni hatua kubwa kuelekea kuisimamisha Urusi,” Mateusz Morawiecki aliandika kwenye Twitter.

Habari Zifananazo

Back to top button