Ukaguzi wataalamu wa ununuzi serikalini waja

WIZARA ya Fedha na Mipango inajenga mfumo mpya wa kielektroniki wa ununuzi wa umma, huku ikifanya ukaguzi katika taasisi zote kubwa za serikali ikiwemo TANESCO, TANROADS na TPA.

Akizungumza Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi  (PSPTB), Godfred Mbanyi, amesema kumekuwa na udhaifu mwingi katika michakato ya ununuzi kwenye taasisi za umma kupitia mfumo wa awali wa TANePS

” PSPTB  tutaanza  ukaguzi kuanzia Septemba 13, 2022 kwenye taasisi za umma na binafsi, ili kuangalia wataalamu wanaofanya kazi za ununuzi maeneo ya kazi, kama wamesomea na kama wana vigezo vingine vya kitaaluma na  kama wamesajiliwa,” amesema Mbanyi.

Amesema hiyo ni  kutokana na changamoto ambazo wamekuwa wakizipata kwa baadhi ya taasisi, ikiwemo kufanya manunuzi chini ya kiwango.

“Sisi kama bodi tumepewa wajibu kisheria kwa mujibu wa kifungu cha 7(23) ya mwaka 2007, kuainisha vigezo vya kitaaluma katika utendaji kazi katika tasnia ya ununuzi na ugavi, hivyo kama tukija kwenye Taasisi tukute mtu awe na sifa za chuo, kwenye Bodi awe amefanya mitihani mpaka ngazi fulani na awe amesajiliwa kwa ngazi fulani, ” amesema.

Mbanyi akizungumza mfumo mpya wa kieletroniki wa ununuzi kwa umma amesema, lengo mfumo huo ni

kurahisisha taratibu zake za ununuzi, ili kutekeleza miradi iliyopo, kutoa huduma kwa wananchi na kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza katika mfumo wa awali wa TANePS.

Amesema  katika mfumo huo mpya, wataalamu wote wa sekta ya umma na binafsi wanatakiwa kujisajili katika mfumo huo mpya wa PSPTB na ambao hawatajisajili, hawataruhusiwa  kufanya kazi zote za ununuzi na ugavi.

“Mfumo umejengwa kwa minajili kwamba hutaruhusiwa kutoka hatua moja kwenda nyingine mpaka uwe umeainisha usajili wako wa bodi, mfumo wameunganishwa na kanzi data ya PSPTB,”amesema

Amesema miongoni mwa changamoto ambazo zilikua zikijitokeza ni mtaalamu yoyote ambaye anafanya kazi za ununuzi wa umma hata kama hatambuliki na bodi alikuwa na uwezo wa ku ‘access’ mfumo na kufanya shughuli za ununuzi.

 

Habari Zifananazo

Back to top button