“Ukamataji wakulima Kahawa waangaliwe upya”

MBUNGE wa Jimbo la Muleba Kusini, Dk Oscr Kikoyo amewaomba Mkuu wa Wilaya ya Muleba na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba kuangazia upya swala la ukamataji wa wakulima wanaovuna Kahawa kutoka mashambani na kupeleka nyumbani kuanika.

Alisema kuwa katika msimu wa kuvuna kahawa kumekuwa na hongezeko la doria mpaka mashambani na kufanya wanachi kukosa Uhuru hata wa kutoa Kahawa yao shambani ambayo wakulima wenyewe wamehiangaikia ambapo alilitaja gari la usajili STK 814 ambalo linafanya doria katika wilaya hiyo na kukamata wakulima wanaotoka shambani kuvuna kahawa.

Advertisement

Kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Muleba Mjini na kuwashirikisha Wananchi aliwahakikishia kuwa serikali ilishatoa kauli juu ya maswala ya kuvuna Kahawa na kuuza,  hivyo Wananchi wapewe uhuru katika mazao.

“Swala la kahawa katika wilaya ya Muleba ni swala la kiuchumi na siasa ,mkulima anapolima anapopanda hakuna anapoangaliwa wala kuulizwa lakini haya magari ambayo yanakamata wakulima kutoka mashambani ni ya nini,je Kahawa itatokaje shambani na kuanikwa ilinipelekwe Sokoni ?? Je Sheria inayolinda wakulima wa mazao mengine kwa Nini isilinde mkulima wa zao la kahawa ?! Tunapaswa kuweka utaratibu mzuri kwa wakulima wetu ili wajisikie huru katika Taifa lao.” alihoji Kikoyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Dk Peter Nyanja alisema kuwa swala la kuvuna limewekewa utaratibu mzuri kuwa lazima kila mkulima wa kahawa anapomaliza kuvuna na kuhanika kahawa zake anapaswa kupeleka katika chama chake cha msingi huku wafanyabiashara wote wakipaswa kununua kahawa kwa njia ya mnada kupitia bodi ya kahawa katika vyama vya msingi .

Alisema tangu kufunguliwa kwa msimu wa mwaka 2023/2024 tayari wameishakamata gari mbili za kahawa ambazo hazikuwa na maelezo juu ya ununuzi wa kahawa wala vibali vya usafirishaji wa Kahawa .


Alisema wafanyabiashara wanaonunua kahawa kwa njia za panya bila kupitia mnada wanakwepa Kodi na lazima serikali iwe na wasiwasi juu ya kuzipata kahawa hizo kwa sababu lengo ni kukusanya mapato ya Halmashauri na tayari amepanga kukutana na wafanyabiashara wa zao la kahawa pamoja na baadhi ya wakulima ili waweze kupatiwa utaratibu unaotakiwa katika kuvuna, kusafirisha na kuuza Kahawa.

3 comments

Comments are closed.