Ukame kuathiri halmashauri  6 Tanga

HALMASHAURI sita za mkoa wa Tanga, zipo hatarini kukabiliwa na upungufu wa chakula na maji kutokana na hali ya ukame iliyosababishwa na kuchelewa kwa msimu wa mvua za vuli, jambo ambalo linaweza kusababisha baa la njaa

Hayo yamesemwa na mratibu wa kudhibiti maafa ya mkoa wa Tanga, Gloria Malewa, wakati wa kikao kazi cha kuandaa mpango mkakati wa kukabiliana na njaa mkoani humo.

Amezitaja halmashauri hizo kuwa ni Mkinga, Kilindi, Handeni, Handeni Mji, Korogwe Mji pamoja na Korogwe.

Aidha amesema kuwa hali hiyo imesababisha kupanda Kwa bei ya mazao huku baadhi ya jamii zenye hali duni kukumbwa na changamoto ya uhitaji wa chakula.

“Tumeanza kuona matukio ya uvamizi wa wanyama pori kama tembo katika makazi ya watu, vyanzo vya maji kukauka hiyo yote ni dalili ya ukame,”amesema Malewa.

Naye mratibu wa mradi wa chakula kutoka shirika la Save The Children, Anania Yusto amesema kuwa wao kama wadau, wapo kwa ajili ya kusaidiana na serikali katika kuweka mipango endelevu ya kusaidia kupambana na janga hilo.

Habari Zifananazo

Back to top button