Ukame wakwamisha uwekaji mifugo hereni za kielektroniki

Ukame wakwamisha uwekaji mifugo hereni za kielektroniki

UWEKAJI hereni za kieletroniki kwa mifugo kwenye wilaya za Mkoa wa Arusha halitafanikiwa kwa sababu ya ukame unaozikabili wilaya mbalimbali na kusababisha mifugo kupelekwa mikoa ya Tanga, Manyara na hata Kenya kwa ajili ya kutafuta malisho

Akizungumza jana katika kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Arusha (RCC), Naibu Waziri wa  Madini, Dk,Steven Kiruswa,  alisema suala hilo halitafanikiwa na kuiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuongeza muda zaidi badala ya kuisha Oktoba 31,mwaka huu.

Amesema ukame umesababisha wafugaji kuhama na mifugo, wengine kuipeleka Kenya,Tanga ,Manyara na mikoa mbalimbali, ili iweze kupata malisho na maji kutokana na janga la ukame, hivyo kwa wafugaji ambao wamehama maeneo yao halitafanikiwa kama wizara iangalie jambo hilo.

Advertisement

Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ilitangaza suala la utambuzi wa mifugo kwa kutumia hereni za kieletroniki kumalizika Oktoba 31 mwaka huu, baada ya hapo wafugaji watatozwa faini.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *