Ukiambiwa HabariLEO Gwiji la Habari usibishe!

DSM; Mwandishi wa gazeti la HabariLEO na DailyNews Digital, Aveline Kitomary ameibuka mshindi wa jumla katika Tuzo ya Mwandishi wa Habari Bora wa uandishi wa habari za dawa,vifaatiba, vitendanishi na bidhaa za tumbaku.

Tuzo hizo zimetolewa leo Septemba 22,2023 kwa mara ya pili na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), ambapo mwaka 2022 Kitomary aliibuka kuwa mshindi kipengele cha magazeti.

Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo hizo, Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Adam Fimbo aliwapongeza waandishi walioibuka washindi na kusema kuwa tuzo hizo ni sehemu kubwa ya jitihada wanazoonesha waandishi wa habari katika kuripoti habari za dawa,vifaa tiba, bidhaa za tumbaku na vitendanishi.

“Tuzo hizi ni kwa ajili ya kutambua kazi kubwa inayofanywa na waandishi wa habari katika kutoa elimu kuhusu dawa, vifaa tiba na bidhaa za tumbaku, hivyo tunatambua mchanga wao mkubwa, “ameeleza Fimbo.

Amewahimiza waandishi wa habari kuendelea kuelimisha jamii bila kuchoka kwani wana nafasi kubwa ya kuwafikia na kuaminika zaidi.

Kwa Upande wake Kitomary amesema siri ya mafanikio hayo ni kufanya kazi kwa bidii na kujituma huku akiwashukuru wahariri wa HabariLEO na Dailynews Digital na waandishi wenzake kwa ushirikiano mkubwa wanaompa, hivyo kuthibitisha kauli mbiu ya gazeti hilo inayosema Gwiji la Habari Tanzania..

“Namshukuru Mungu na ninafurahi sana na kuibuka mshindi wa jumla matokeo haya, yote ni ushirikiano mkubwa kutoka kwa wahariri wangu ,waandishi na vyanzo vya habari, wanamchango mkubwa katika hili nawashukuru sana,”amesisitiza Kitomary.

Msindi wa pili katika tuzo hizo ni Marry Geofrey wa gazeti la Nipashe, huku mshindi wa tatu akiwa ni Philip Mwihava wa Redio Clouds.

Habari Zifananazo

Back to top button