Ukiingia Zanzibar hutoki!

NAIBU Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango wa Zanzibar,  Ali Suleiman Ameir amesema mwekezaji yeyote atakayeingia Zanzaibar, hatoki kutokana na fursa lukuki za uwekezaji zilizopo.

Amesema uwekezaji kwenye sekta ya utalii na uchumi wa buluu, ni miongoni mwa fursa hizo, hivyo jicho la mwekezaji yeyote lijikite kwenye maeneo hayo ambayo yanakua kila mwaka.

Ameyasema hayo kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaa ‘SabaSaba 2023’, wakati wa maadhimisho ya siku ya Zanzibar.

Aidha, amesema amesema ni wajibu kuenzi utamaduni wa Zanzibar kwani utamaduni wa Zanzibar ni utambulisho ni siasa pia uchumi wa Zanzibar.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button