Ukimheshimu Lowassa anakuheshimu- Samia

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema miongoni mwa vitu alivyojifunza kutoka kwa hayati Edward Lowassa ni kiongozi ambaye ukimheshimu anakuheshimu pia.

“Nilijifunza mengi kutoka kwake (hayati Edward Lowassa). Kati ya hayo, nililoliona kwa mheshimiwa Lowassa ni kwamba ukimheshimu, anakuheshimu.” – Rais Samia Suluhu katika ibada ya mazishi ya   Lowassa

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Februari 17, 2024 wakati akitoa neno la pole kwa familia ya aliyekuwa Lowassa wakati wa maziko yake kijijini kwake Ngaresh wilayani Monduli, mkoani Arusha.

Pamoja nna hilo,Rais Samia amesema Lowassa hakuwahi kuwasema vibaya wapinzani wake wa kisiasa pindi alipoamua kuhama chama.

Habari Zifananazo

Back to top button