‘Ukiukwaji sheria umekwamisha urasimishaji makazi Dar’

UKIUKWAJI wa sheria za upimaji na urasimishaji ambao umefanywa na kampuni za upimaji na urasimishaji jijini Dar es Salaam ni moja ya changamoto zilizotajwa kusababisha suala hilo kushindwa kufikia malengo, ikiwa imesalia miezi 11.

Urasimishaji maeneo kwa wananchi lilianza mwaka 2013, ikiwa ni mradi wa miaka 10, ukitarajiwa kukamilika mwaka huu 2023.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika kikao kazi cha kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazokwamisha  urasimishaji, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angelina Mabula amesema kumekuwepo na matumizi makubwa ya fedha za mradi huo,unaofanywa na kampuni husika kuchukua fedha za wananchi na kutofanya kazi.

“Orodha tunayo kuna waliokusanya pesa vizuri kazi hawakufanya mwananchi anabaki analia pesa yake imeshachukuliwa, akienda kwa Mkurugenzi hana habari kwa sababu mikataba haijui, akija wizarani, wizara haina habari kwa sababu ni mamlaka za upangaji, inakuwa ni danadana huku na huku na pesa yake ishaondoka,” amesema Dk Mabula.

Amesema Jiji la Dar es Salaam lina asilimia 24 ya kazi yote ya urasimishaji nchini, na mpaka sasa imefanya kwa asilimia 20 tu, ikiwa wamepanga viwanja 554,783 na kuwasilishwa kupitia michoro 2084.

Akitaja hatua ambazo wizara imezichukua Dk Mabula amesema wamezuia na kusitisha mamlaka za upangaji kutoa kandarasi mpya za urasimishaji wa kampuni binafsi za urasimishsji na upimaji kwa lengo la kupisha tathimini ya miradi iliyokuwa inaendelea.

“Kampuni 15 zimechukuliwa hatua, kampuni 7 za upangaji na upimaji zimefungiwa, kuingia mikataba mipya na kandarasi, kampuni sita zimepewa onyo, na Kampuni kumi zimesitishiwa mikataba ya kandarasi za urasimishaji na mamlaka za upangaji,” amesema.

Katika mkutano wake huo ambo umewashirikisha wadau wa ardhi wakiwemo mameya, wakuu wa wilaya, maofisa ardhi, makamishna, wakurugenzi pamoja na wamiliki wa kampuni za upangaji na upimaji, Dkt. Mabula akataka ufutwaji wa umiliki wa meneo yote ambayo ni mapor,i ili yaweze kupangiwa matumizi mengine.

“Unapompa mtu kiwanja ndani yake kuna masharti, eneo la makazi miezi 36 liwe limeendelezwa, kuna viwanja miaka 20,30, 40, havijaendelezwa, maeneo mengine yanamilikiwa na taasisi za umma, tunasema bila kujali linamilikiwa na nani kama masharti hayakufuatwa, taratibu za kunyang’anywa zifuatwe.”

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x